~~ Mishono hot hot ya kitenge kama kawa ~~

Kifupi kitenge ni sawa na mchele. Kwamba mchele mmoja lakini mapishi ni mengi. Kila mmoja na upishi wake. Vivyo hivyo kwa kitenge. Kitenge ni kimoja lakini kila mmoja hukishona apendavyo. Waweza shona gauni, sketi na blauzi, suruali na hata kaptula. Wala hugombwi ili radi roho yako imependezwa nao.